| AJIB |
Wakati
Simba ikitarajiwa kukipiga na Stand United kesho Jumamosi mkoani
Shinyanga, mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajib, amesema kuwa mechi ngumu
iliyobaki kwao ni Yanga kutokana na wachezaji wa timu zote kukamiana.
Februari
20, mwaka huu, Simba na Yanga zitakutana katika mechi ya raundi ya pili
ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo Simba
itakuwa chini ya Kocha Jackson Mayanja ambaye ameiongoza timu hiyo
kushinda mechi sita mfululizo.
Ajib
amekuwa katika kiwango cha juu kwa hivi sasa huku akiwa ameshafunga
mabao nane katika ligi kuu, hivyo anaweza kuwa mchezaji muhimu katika
mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Ajib
alisema wanachokiangalia ni ushindi tu katika kila mechi iliyopo mbele
yao lakini anaamini mechi yao dhidi Yanga itakuwa ngumu tofauti na watu
wanavyofikiria.
“Yanga
ni timu nzuri kutokana na aina ya wachezaji wao, imebakia mechi hiyo
ambayo naamini itakuwa ngumu sana kwa sababu kila timu itakuwa inahitaji
matokeo ya ushindi lakini timu yetu ipo vizuri na hatuwezi kuwahofia
kwa sababu malengo yetu ni kushinda kila mchezo.
“Waje
tu, kazi itaonekana kati yetu nani anastahili ushindi, ingawa dakika 90
ndizo zitatoa majibu ya kweli, tusubiri tuone itakuwaje,” alisema Ajib.

Hakuna maoni :