Bosi
wa Simba katika benchi la ufundi, Jackson Mayanja, ametamba kuwa
anasubiri ushindi mmoja tu katika mchezo ujao dhidi ya Yanga ili aweze
kuamini kuwa wana asilimia kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara
msimu huu.
Baada
ya ushindi wa juzi dhidi ya Stand United ugenini, Mayanja ya Simba
imeshinda mechi zote saba ilizocheza, ikiwemo ya Kombe la FA dhidi ya
Burkina Faso.
Mayanja amesema mchezo ujao dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga, ndiyo utamfanya atangaze ubingwa.
“Kwanza
yote kwa yote namshukuru Mungu kuniwezesha kupata matokeo mazuri tangu
nijiunge na Simba na hii inatokana na ushirikiano mzuri ninaoupata
kutoka kwa viongozi wangu pamoja na wachezaji kufuata maelekezo
ninayowapa katika mazoezi ambayo yanawasaidia kucheza soka la kuvutia na
kupata matokeo mazuri.
“Katika
mechi zilizobaki, mechi ngumu zaidi itakuwa ni dhidi ya Yanga ambayo
naamini kama tutashinda, basi nitatangaza nafasi ya ubingwa, kwa kuwa
tukishaiacha Yanga pointi nyingi, tunakuwa katika nafasi nzuri zaidi,”
alisema Mayanja.
Simba
itacheza na Yanga Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikiwa
mbele yao kwa tofauti ya pointi mbili huku Yanga ikiwa na mchezo mmoja
mkononi.

Hakuna maoni :