![]() |
| AFRICA LYON ILIYOKUWA LIGI KUU KABLA YA KUPOROMOKA |
African
Lyon ya jijini Dar, jana Jumapili ilifanikiwa kurejea tena ligi kuu,
kufuatia sare ya bao 1-1 dhidi ya Ashanti United katika mchezo wa mwisho
wa Ligi Daraja la Kwanza uliyopigwa kwenye Uwanja wa Karume, Dar.
Lyon
imemaliza Kundi A ikiwa kileleni kwa pointi 27, ikifuatiwa na Ashanti
yenye 24 huku Friends Rangers ikishika nafasi ya tatu baada ya kukubali
kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Kiluvya United katika mchezo wao
uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar, jana.
Lyon
inaungana na Ruvu Shooting kutoka Kundi B, huku kitendawili kikibaki
kwa Kundi C baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kusema
halitaitangaza timu iliyopanda ligi kuu kati ya Geita Gold Sports na
Polisi Tabora mpaka pale litakapopata ripoti ya waamuzi wa michezo hiyo
kutokana na jinsi matokeo yake yalivyokuwa na utata.
Mbali
na timu zilizopanda, kwa upande wa pili, timu za Mji Mkuu kutoka
Dodoma, Burkinafaso (Morogoro) na JKT Kanembwa ya Kigoma zimeshuka
daraja kutoka ligi hiyo.


Hakuna maoni :