SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / MASHABIKI WAMVAA WENGER BAADA KUANZA 2016 HOI NA KUTUPWA WA 4.

LIGI KUU ENGLAND
Matokeo:
Jumanne 2 Februari 2016
Arsenal 0 Southampton 0           
Leicester 2 Liverpool 0               
Norwich 0 Tottenham 3              
Sunderland 0 Man City 1            
West Ham 2 Aston Villa 0           
Crystal Palace 1 Bournemouth 1           
Man United 3 Stoke 0                 
West Brom 1 Swansea 1   

ARSENAL-WENGER-KIDOLEBAADA ya Jana kutoka Sare 0-0 na Southampton Uwanjani Emirates matokeo ambayo yamewatupa hadi Nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu England, Mashabiki wa BPL-FEB3Klabu hiyo wamemjia juu Meneja wao Arsene Wenger na kudai hajui afanyalo huku mwenyewe akikiri sasa mambo ni magumu kwao.


Sasa Arsenal hawajashinda katika Mechi za Ligi 4 na wametupwa Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 5 nyuma ya Vinara Leicester City.

Wakichemka kwenye Mitandao ya Jamii, na hasa Twitter, Mashabiki wa Arsenal wamemponda Arsene Wenger na kumsema ‘Sasa hajui afanyalo katika kila Gemu!’.

Akiongea baada ya Sare na Southampton, Wenger alisema: “Inabidi tuwakimbize Vinara na tuna program ngumu. Inabidi tujibu kwenye Gemu za Ugenini!”


Arsenal wameshinda Mechi 1 tu ya Ligi Mwaka huu na kisha kutoka 3-3 na Liverpool huko Anfield, 0-0 huko Stoke na kufungwa 1-0 kwao Emirates na Chelsea na kufuatia hii Sare na Southampton.


Alipohojiwa kama sasa Msimu wa Arsenal umefifia na wameanza kupotea kwenye mbio za Ubingwa, Wenger alijibu: “Ni mapema mno kusema hilo. Ni kweli tumeanza kwa kusuasua 2016.”


PATA BAADHI YA POSTI ZA TWITTER:
ARSENAL-TWITTER
Arsenal – Mechi ngumu za Ugenini:
Bournemouth v Arsenal (Ligi Kuu England, 7 Februari)
Man Utd v Arsenal (Ligi Kuu England 28 Februari)
Tottenham v Arsenal (Ligi Kuu England 5 Machi)
Barcelona v Arsenal (UEFA CHAMPIONZ LIGI, Marudiano Raundi ya Mtoano, 16 Machi)
Everton v Arsenal (Ligi Kuu England, 19 Machi)
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba
Jumatano 3 Februari 2016
[Mechi kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku]
Everton v Newcastle         
Watford v Chelsea

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply