Pamoja na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Simba kuonekana ni mtamu kwa mashabiki wa Yanga, wao ndiyo waliongoza kwa kuzimia.
Mashabiki 18 walizimia kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kutibiwa hiyo jana huku wa Simba wakiwa ni nane tu.
Mmoja wa wahudumu wa Vijana wa Skauti alisema mashabiki waliokuwa na jezi za rangi ya njano ndiyo walikuwa wengi zaid.
“Wengine
tuliwapatia huduma palepale walipokuwa, lakini wengine tulisaidiana na
watu wa huduma ya kwanza na kuwapeleka ndani,” alisema lakini
akasisitiza yeye si msemaji.
Katika
mechi hiyo mashabiki wengi wa Simba walijitokeza huku wakionyesha
kuiamini zaidi timu yao iliyokuwa imecheza mechi sita za ligi bila ya
kupoteza hata moja.
Lakini
bao moja katika kila kipindi baada ya beki wake Abdi Banda kuwa
amelambwa kadi nyekundu, lilifanya waone kama hawaamini kilichokuwa
kikitokea huku wa Yanga waliokuwa na hofu ya kipigo, walionekana
kuzidiwa na furaha.

Hakuna maoni :