Baada
ya Azam FC kuitwanga Mbeya City kwa mabao 3-0 jana, Kocha Mkuu wa
kikosi hicho kutoka Chamazi, Stewart Hall amesema bado wako kwenye nguvu
za ubingwa.
Hall raia wa Uingereza amesema wana nafasi ya kuendelea kupigania ubingwa kwa kuwa wana kikosi bora.
“Katika
mpira hauwezi kwenda moja kwa moja tu, ikitokea hivyo ujue ni mara
chache sana. Lakini sisi bado tuko kwenye mbio za ubingwa.
“Wakati
mwingine ni shida kidogo kwa kuwa ukiteleza kidogo watu wanakuwa na
maneno hadi yanachanganya. Lakini hakukati tamaa,” alisema.
Azam
FC imerejea katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 45 sawa na Simba
iliyo katika nafasi tatu. Vinara sasa ni Yanga wakiwa na pointi 46.
Azam
FC inaonekana kuwa na advantage zaidi kwa kuwa ina viporo vya mechi
mbili ukilinganisha na Simba, kiporo cha mechi moja ukilinganisha na
Yanga.

Hakuna maoni :