Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata
magari mawili yakihusishwa na wizi katika ofisi ya kamshina mkuu wa TRA
huku yakiwa na vifaa vilivyoibiwa katika ofisi hiyo vikiwa ni pamoja na
komputa na TV.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kamanda
wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema kutokana na
oparasheni kali iliyokuwa ikiendeshwa na jeshi ilifanikiwa kuwatia
nguvuni watuhumiwa wanne wakiwa na vifaa vilivyoibiwa.
Ameyataja magari hayo kuwa ni Toyota Noah yenye namba za usajili T 989
CNV na Mitubish Pajero yenye namba za usajili T 386 CVV .Pia walinzi
wawili waliokuwa zamu kulinda siku hiyo wamekamatwa.
"Katika wizi huo vitu vilivyoibwa ni Compyuta mbili, aina ya Dell pamoja na CPU, Monitor zake na Televisheni moja aina ya Sumsung inchi 40" Alisema Sirro.
Aidha kamanda huyo wa kanda maalum ya Dar es Salaam amesema katika
oparesheni hiyo pia jeshi la polisi lilifanikiwa kuokoa zaidi ya
shilingi milioni 150 mali ya Bw Ahmed Huwel mkazi wa Msasani.
Katika hatua nyingine kamanda Sirro ametangaza kusitishwa kwa muda kwa
shughuli za ulinzi shirikishi katika vituo vya polisi kutokana na
vikundi hivyo kualamikiwa na wananchi kwa kutokuwa na tija katika jamii
Hakuna maoni :