SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / SIMBA WAPIGA DUA YA "KATARINA NJOO, MVUA USIJE", UNAJUA NI KWA NINI.


Simba wako tayari kwa ajili ya mechi ya Stand United, lakini wanachoomba ni dua ya kuzuia mvua kwa kuwa wanaijua shughuli yake.

Enzi la utoto, kulikuwa ule wimbo wa “Katarina njoo, mvua usije”, kuzuia mvua isinyeshe.

Huenda Simba watakuwa wanaimba wimbo huo kimyakimya ili kuepusha kutonyesha kwa mvua hasa Jumamosi.

Simba itakuwa kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga kuwavaa wenyeji wake Stand United.

Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Simba, Haji Manara amesema dua yao kuu ni mvua isinyeshe.

“Ikinyesha mvua, uwanja unakuwa tatizo kabisa. Tunaomba angalau Jumamosi isinyeshe ili uwanja uwe vizuri.

“Tunatamani hivyo ili tuweze kupata nafasi ya kucheza mechi nzuri na kuwaonyesha watu tulichonacho lakini kupambana pia kupata ushindi.

“Hadi sasa hapa Shinyanga hali ni nzuri na maandalizi ni mazuri kabisa,” alisema Manara.

Tayari Simba imecheza mechi moja kwenye uwanja huo baada ya kuishinda Kagera Sugar kwa bao 1-0.


Sasa inasubiri kucheza dhidi ya wenyeji hao ambao ni timu iliyoanzishwa na wapiga debe wa mabasi yanayotoka au kupita Shinyanga mjini kwenda sehemu nyingine za mkoa huo au nje.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply