Mganda Hamisi Kiiza ameonyesha kweli amepania kufanya vema zaidi na kupachika mabao kila inapowezekana kuisaidia Simba.
Kiiza
amefunga mabao mawili leo na kuisaidia Simba kushinda kwa 2-1 dhidi ya
Stand United, sasa ndiyo vinara wa Ligi kuu Tanzania Bara baada ya
kufikisha pointi 44.
Mabao
hayo mawili, yamekuwa msaada kwa Simba lakini msaada kwa Kiiza ambaye
amefikisha mabao 16 na kumpita mshindani wake mkuu katika upachikaji
mabao, Amissi Kiiza wa Yanga mwenye 14.
Kiiza
alikuwa akiitumikia Yanga nchini Mauritius katika mechi ya Ligi ya
Mabingwa Afrika. Kuna nafasi ya kufunga katika mechi ijayo lakini tayari
Kiiza aliyekuwa nyuma yake kwa mabao manne, sasa amempita.
Donald Ngoma ana mabao 10 sawa na Jeremiah wa Prisons na Elius Maguri wa Stand United ana 9 akiwa amekwama hapo muda mrefu sasa.

Hakuna maoni :