LIGI KUU ENGLAND
Ratiba/Matokeo:
Jumamosi 13 Februari 2016
Sunderland 2 Man United 1
[Mechi kuanza Saa 12 Jioni]
Bournemouth v Stoke
Crystal Palace v Watford
Everton v West Brom
Norwich v West Ham
Swansea v Southampton
2030 Chelsea v Newcastle
Katika
Mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England hii Leo iliyochezwa huko Stadium of
Light Wenyeji Sunderland wameichapa Man United Bao 2-1.Sunderland walitangulia kupata Bao Dakika ya 3 tu baada ya Frikiki ya Wahbi Khazri kupenya chini na kumshinda Kipa David de Gea.
Man United walisawazisha Dakika ya 39 kufuatia Shuti la Juan Mata kutemwa na Kipa Mannone na kumfikia Anthoby Martial aliefunga kifundi.
Bao hizo zilidumu hadi Mapumziko.
Sunderland walifunga Bao lao la pili Dakika ya 82 kwa Kichwa cha Lamine Kone baada ya Mpira wa Kona kuokolewa mstarini na Martial na kumgonga Kipa De Gea na kutinga.
Hadi mwisho Sunderland 2 Man United 1.
VIKOSI:
Sunderland: Mannone, Yedlin, Kone, O’Shea, Kirchhoff, Van Aanholt, M’Vila, Cattermole, Khazri, Defoe, N’Doye.
Akiba: Brown, Rodwell, Borini, Matthews, Pickford, Toivonen, Honeyman.
Manchester United: De Gea, Darmian, Smalling, Blind, Borthwick-Jackson, Carrick, Schneiderlin, Lingard, Mata, Martial, Rooney.
Akiba: Depay, Romero, Ander Herrera, Andreas Pereira, Weir, Keane, Love.
REFA: Andre Marriner
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba
Jumapili 14 Februari 2016
1500 Arsenal v Leicester
1705 Aston Villa v Liverpool
1915 Man City v Tottenham

Hakuna maoni :