Michuano
ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) inatarajiwa
kuendelea wiki hii mzunguko wa nne katika hatua ya 16 bora, kwa michezo
nane kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini.
Jumatano
Februari 24, 2016 kutakua na mchezo mmoja tu, ambapo timu ya Young
Africans watawakaribisha maafande wa JKT Mlale kutoka mkoani Ruvuma
katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, mchezo utakaochezwa majira
ya saa 10:30 jioni.
Michezo
miwili itachezwa siku ya Ijumaa ambapo, Ndanda FC watakua wenyeji wa
JKT Ruvu katika uwanja wa Nagwanda Sijaon mjini Mtwara, huku Coastal
Union wakiwakaribisha wakata miwa wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga.
Jumamosi
Februari 27, Mwadui FC watawakaribisha maafande wa Rhino Rangers katika
uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga, wakati jijini Mbeya Tanzania
Prisons watacheza dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Sokoine jijini
humo.
Mzunguko
huo wa nne utakamilika siku ya Jumapili ambapo, Simba SC
watawakaribisha Singida United katika uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam, Panone FC dhidi ya Azam FC uwanja wa Ushirika mjini Moshi, huku
Toto Africans wakicheza dhidi ya Geita Gold katika uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza.

Hakuna maoni :