| UGANDO KAZINI... |
Kiungo kinda wa Simba, Hija Ugando ni majerudi na atakaa nje kwa wiki mbili kabla ya kurejea uwanjani.
Ugando
ambaye alianza kuaminiwa na Kocha Jackson Mayanja ameanza kwa kuikosa
mechi dhidi ya Yanga ambayo Simba ililala kwa mabao 2-0.
“Kweli
Ugando atakuwa nje kwa wiki mbili, ni jambo la kusikitisha kwetu kwa
kuwa tulikuwa tunamhitaji zaidi kipindi hiki,” kilieleza chanzo cha
uhakika.
Ugando tayari alionyesha mwelekeo mzuri tokea aanze kupewa nafasi ya kucheza na Mayanja raia wa Uganda.

Hakuna maoni :