Makamu
wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, amesema kocha wa kikosi
chao, Jackson Mayanja, amejitahidi kwa kiasi kikubwa kubadili mambo hata
kuliko ilivyokuwa kwa makocha Wazungu waliopita Simba.
Kaburu alisema kuwa Mayanja amebadili mambo mengi katika
saikolojia kwa wachezaji, lakini hali ya utimilifu wa mwili, hivyo ni
jambo jema kumuacha aendelee na anachokifanya huku uongozi ukibaki nyuma
yake na kumuunga mkono.
“Hakika
amejitahidi sana, angalia timu inavyocheza kwa kupambana kwa dakika
zote 90. Timu ina nguvu na kasi, hakika wanacheza vizuri.
“Kama
unakumbuka, Simba tulikuwa tunapambana kipindi cha kwanza na kufanya
vizuri. Tukiingia kipindi cha pili mabao yote yanarudi.
“Kama
uongozi tunamuunga mkono kocha na wachezaji wote kwa asilimia mia na
moja. Tunamuacha aendelee kuongoza kikosi chake huku akipata sapoti
yetu.
“Kama
uongozi, hatuwezi kukaa tu kimya, badala yake kwenye ushauri tutashauri
na tutashirikiana na wote. Hongera kwake, pia kwa wachezaji,” alisema
Kaburu.
“Kazi
ya Mayanja ni kuzidi hata ya makocha Wazungu. Wachezaji kuipatia klabu
ubingwa ni wajibu wao. Uongozi pia tutakuwa karibu yao ili waendelee
kupambana.”
Simba kwa sasa iko kileleni mwa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 54 ikiwa inafuatiwa na Yanga yenye pointi 50 na Azam FC pointi 47.
Wakati
Simba imecheza mechi 23, Yanga imecheza mechi 21 na Azam FC imecheza
20. Timu hizo zinategemea viporo vyake ili kuikamata Simba.
Hakuna maoni :