• Manchester City (4-2-3-1): Hart 7, Maffeo 6.5, Stones 7 (Adarabioyo 60, 6)...

  • SALVATORY EDWARD Kiungo wa zamani wa timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kide...

  • Baada ya kikosi cha Mwadui FC kuchapwa kwa bao 1-0 katika mechi yao ya Lig...

  • Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeweka bayana kuwa, lipo kwenye mpango wa ...

SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / KABURU: SIMBA NA KESSY KILA KITU SAFI KABISA, KASORO.


KABURU

Uongozi wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam umesema umefika mbali katika suala lake na beki wake, Hassan Kessy na una imani kubwa ataendelea kubaki na kuitumikia klabu hiyo msimu ujao.

Makamu Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema wameanza mazungumzo na Kessy na yako katika hatua nzuri sana.

“Tuko katika hatua nzuri sana ya mazungumzo. Tumeanza mazungumzo kipindi sasa na tuna matumaini makubwa Kessy ataendelea kubaki Simba,” alisema Kaburu.
KESSY

“Tunaamini Kessy tunamhitaji, naye ni kijana anayeipenda Simba. Hivyo tukifikia makubaliano, tutaingia mkataba na kuwataarifu.”

Kumekuwa na taarifa huenda Kessy ana mpango wa kujiunga na Yanga hali iliyoonyesha kuwaudhi baadhi ya mashabiki wa Simba.


Hata hivyo kumekuwa na mgawanyiko kuhusiana na beki huyo wa kulia mwenye uwezo wa kupiga krosi nyingi. Wengine wakisema abaki na wengine wakikubali aende zake.

«
Next
SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya March 16, Ikiwemo ya Lowassa Kung'oa Vigogo CCM.
»
Previous
BARCELONA V ARSENAL JUMATANO - KUIFUNGA ARSENAL EMIRATES SI TIJA, BARCA WASEMA ‘HAPA KAZI TU.

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply