KERR |
Aliyekuwa
Kocha wa Simba, Muingereza, Dylan Kerr, bado anaifuatilia Ligi Kuu Bara
na amesema kutokana na Yanga na Azam kushiriki michuano ya kimataifa,
Simba ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa msimu huu.
Kerr aliiacha Simba ikiwa nafasi tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, kwa sasa timu hiyo ndiyo inaongoza ligi.
Yanga
na Azam juzi Jumamosi zilishinda mechi zao za kimataifa, Yanga
iliifunga APR ya Rwanda mabao 2-1 kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, huku
Azam ikiichapa Bidvest Wits ya Afrika Kusini mabao 3-0 katika Kombe la
Shirikisho Afrika.
Kerr
anaamini Yanga na Azam zitakuwa zikitolea macho zaidi michuano ya
kimataifa huku wachezaji wake wakitumika sana na hiyo ndiyo itawafanya
Simba kufanya vizuri na hatimaye kuwa mabingwa.
“Unapokuwa
unashiriki michuano mingi, mara chache sana unaweza kufanikiwa kufanya
vizuri kote, lakini timu nyingi hushindwa kumudu na kujikuta zikipoteza
kote.
“Hali
hiyo kwa sasa ndiyo wanayo Yanga na Azam ambazo zinawania ubingwa wa
ligi na Simba, zenyewe zinashiriki michuano zaidi ya miwili wakati Simba
yenyewe inashiriki miwili tu (ligi na Kombe la FA), kwa maana hiyo
naona kabisa Simba ndiyo ina nafasi kubwa ya kuwa bingwa wa ligi msimu
huu kuliko hizo nyingine,” alisema Kerr.
Hakuna maoni :