Azam
FC imesonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho kwa kuifunga
tena Bidvest ya Afrika Kusini, safari hii kwa mabao 4-3.
Katika
mechi ya kwanza, Bidvest ilipoteza kwa mabao 3-0 ikiwa nyumbani
Johannesburg. Safari hii imepata imepata mabao matatu lakini
ikashindiliwa mengine manne. Maana yake Azam FC imevuka kwa jumla ya
mabao 7-3.
Mshambuliaji
wa Azam FC, Kipre Tchetche amefunga mabao matatu, hat trick na moja
likapachiwa na nahodha wake, John Raphael Bocco.
Hata hivyo, Azam FC ilishindwa kuonyesha kiwango kizuri hasa katika ulinzi huku beki wake kisiki, Serge Wawa akionekana kupwaya.
Kwani
pamoja na washambuliaji wake kufunga mabao manne, lakini safu ya ulinzi
ya Azam FC ilionekana kutokuwa imara huku Bidvest wakifunga kwa ulaini
kutokana na soka lao la kitabuni.
Bidvest waliotumia vijana zaidi, walicheza soka la kitabu au la kufundishwa zaidi na kufanya kila jambo lao kuonekana rahisi.
Azam FC nao walionyesha soka safi hasa kipindi cha kwanza, lakini mambo yalizidi kubadilika kila wanavyosonga mbele.
Hakuna maoni :