SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / KWA MAKUNDI, TAIFA STARS YATUA SALAMA SALIMINI CHAD TAYARI KUWAVAA WENYEJI.



Timu ya soka ya taifa, Taifa Stars imewasili salama salimini mjini  N'Djamena tayari kuwavaa wenyeji Chad kati mechi ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2017.

Taifa Stars inayonolewa na kocha mkuu Charles Boniface Mkwasa akisaidiwa na Hemed Morocco kimewasili D’jamena leo majira ya saa 7 mchana kwa saa za huku kwa shirika la ndege la Ethiopia, sawa na saa saa 9 alasiri kwa saa za nyumbani na Afrika Mashariki na kufikia katika hoteli ya Legder Plaza.


Msafara wa 20 wa kundi la kwanza uliowasili umejumuisha viongozi pamoja na wachezaji 12, huku kundi la pili likitarajiwa kuondoka Tanzania Jumatatu usiku na kuwasili Jumanne kuungana kwa mazoezi ya mwisho nchini humu.

Stars inatarajiwa kufanya mazoezi kesho Jumatatu na Jumanne katika Uwanja wa Omnisports Idrissm Mahamat Ouya kujiandaa na mchezo huo wa Jumatano katika dimba hilo hilo jijini N'Djamena.

Wachezaji waliowasili nchini ni Chad ni Ally Mustafa, Juma Abdul, Haji Mwinyi, kelvin Yondani, Deus Kaseke, Mohamed Hussein, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Ibrahim Ajibu, Shiza Kichuya, Mohamed Ibrahim na nahodha Mbwana Samatta.


Mchezo kati ya Chad dhidi ya Tanzania unatarajiwa kuchezwa siku ya Jumatano Alasiri kwa saa za huku, sawa na saa 11 jioni kwa saa za nyumbani Tanzania.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply