SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / LA LIGA: REAL YAJIKONGOJA, USHINDI DAKIKA ZA MWISHO.


3000Real Madrid wamepata ushindi wao wa 3 mfululizo kwenye La Liga Ugenini huko Visiwa vya Canary walipoichapa Las Palmas 2-1 kwa Bao za Sergio Ramos na Casemiro.
 
Bao la ushindi la Casemiro lilifungwa Dakika ya 89 mara tu baada ya Willian Jose kuisawazishia Las Palmas.
 
Real walimaliza Mechi hii wakiwa Mtu 10 kufuatia Sergio Ramos kupewa Kadi za Njano 2 na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu Dakika za Majeruhi.
Ushindi huu unewabakisha Real Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Mahasimu wao Atletico Madrid.
 
Barcelona, ambao ndio Mabingwa Watetezi, wanaongoza La Liga wakiwa na Pointi 75, Atletico 67 na Real 64 huku Mechi zikibaki 9.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply