Jopo
la madaktari raia wa India, wamekabidhiwa beki wa Yanga, Nadir Haroub
‘Cannavaro’ kusimamia majeraha yake ya kifundo cha mguu ‘enka’.
Hiyo
yote ni katika kuhakikisha anapata matibabu mazuri na haraka ili arejee
uwanjani kuisaidia timu hiyo inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika,
Kombe la FA na Ligi Kuu Bara.
Awali,
beki huyo alikuwa akipatiwa matibabu hayo ya enka kwenye Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya London Health
Centre ya jijini Dar es Salaam inayohusika na masuala ya mifupa.
Cannavaro
alisema baada ya kugundulika hana tatizo kubwa la kusababisha afanyiwe
upasuaji, jopo hilo la madaktari limemuandalia kliniki maalumu chini ya
madaktari raia wa India.
Cannavaro
alisema kliniki hiyo atakayoihudhuria itaenda sambamba na matibabu,
pia programu maalum ya mazoezi kwa ajili ya kuimarisha mifupa yake.
Aliongeza
kuwa, kliniki hiyo ataihudhuria hospitalini hapo kwa muda wa wiki tatu
kabla ya wiki inafuata kuanza mazoezi ya pamoja na wenzake.
“Katika
kupunguza gharama za kwenda kwenye matibabu nchini India, uongozi wa
Yanga umenihamishia kwenye hospitali maalumu inayohusiana na matibabu ya
mifupa pekee ambayo ipo hapa nchini.
“Hospitalini
hapo, huduma inayotolewa ni ya mifupa ambayo tayari nimeanza matibabu
yangu ya enka iliyoniweka nje ya uwanja tangu Novemba.
“Ninahudhuria
kliniki kila baada ya siku tano huku nikifanyishwa mazoezi maalum na
madaktari hao, hiyo yote ni katika kuhakikisha ninapona na ninarejea
uwanjani haraka kuitumikia timu yangu ya Yanga,” alisema Cannavaro.
Hakuna maoni :