Liverpool ikicheza na wachezaji 10 kwa
dakika nyingi uwanjani, imelazimika kutoka nyuma kwa kufungwa bao 1-0 na kupata
ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace katika Ligi Kuu ya England ‘Premier
League’ kwenye Uwanja wa Selhurst Park.
Liverpool ambayo kutokana na ushindi
huo sasa imefikisha pointi 44 na kushika nafasi ya saba katika msimamo wa
Premier, ilicheza pungufu muda mwingi kutokana na kiungo wake mkongwe James
Milner kupewa kadi ya pili ya njano katika dakika ya 63.
James Milner (kushoto) akitoka uwanjani baada ya kupewa kadi nyekundu. |
Crystal Palace ilipata bao lake
katika dakika ya 49 kupita kwa Joseph Ledley wakati ambapo Liverpool
ilisawazisha katika dakika ya 72 kupitia kwa Roberto Firmino.
Bao la pili lilipatikana baada ya Christian
Benteke kuchezewa faulo katika dakika za lala salama kisha yeye mwenyewe
kuutupia mpira wavuni.
Hakuna maoni :