Kocha
Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia
ya Kilimanjaro Premieum Lager, Charles Boniface Mkwasa leo ametangza
kikosi cha wa wachezaji 25 kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu kwa
fainali za Mataifa Afrika (AFCON) dhidi ya Chad, Machi 23, 2016 mjini
Djamena.
Akiongea na waandishi wa habari wakati akitangaza kikosi hicho,
Mkwasa amewaomba wachezaji aliowaita katika kikosi hicho, kujiweka fit
katika mazoezi wanayoyafanya katika vilabu vyao, kwani hakutakua na muda
wa kufanya mazoezi kwa ajili ya mchezo huo wa ugenini.
“Ligi Kuu ya Vodacom, michuano ya CAF (CL, CC) inachezwa wikiendi
ya tarehe 18-20 Machi, hivyo wachezaji wote watakua na majukumu katiak
timu zao, muda wa kufanya mazoezi kwa pamoja kwa ajili ya mchezo huo
hautakuwepo, ndio maana nasisitiza wachezaji niliowachagua wahakikishe
wanajilinda wenyewe kwa kuwa fit wanapokuja kwenye safari ya mchezo huo
wa machi 23, 2016” alisema Mkwasa
Wachezaji walioitwa Taifa Stars ni magolikipa Aishi Manula (Azam
FC), Ally Mustapha (Young Africans) na Shaban Kado (Mwadui FC), walinzi
ni Juma Abdul, Haji Mwinyi, Kelvin Yondani (Young Africans), Shomari
Kapombe, Erasto Nyoni, David Mwantika (Azam FC) na Mohamed Hussein
(Simba SC).
Viungo Himdi Mao (Azam FC), Ismail Juma (JKU), Jonas Mkude, Said
Ndemla, Mwinyi Kazimoto (Simba SC), Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya
(Mtibwa Sugar), Farid Mussa (Azam FC), Deus Kaseke (Young Africans).
Washambuliaji ni Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk), Thomas
Ulimwengu (TP Mazembe), John Bocco (Azam FC), Elias Maguri (Stand
United), Jeremia Mgunda (Tanzania Prisons) na Ibrahim Hajibu (Simba
SC).7
Hakuna maoni :