SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / MTIBWA YAIZAMISHA JKT RUVU YA KIBADENI KWA BAO 2-1.



MTIBWA


Mtibwa Sugar imekusanya pointi tatu nyingine za Ligi Kuu Bara baada ya kuichapa JKT Ruvu kwa mabao 2-1.

JKT inayofundishwa na Kocha mkongwe nchini, Abdallah King Kibadeni, imezidi kudidimia na sasa inabaki na pointi 21 ambazo ni hatari kwake kwa kuwa timu nne chini yake, tofauti ya pointi ni ndogo sana.

Katika mechi ya leo, Mtibwa ndiyo wa kwanza kupata bao kupitia beki wake Salim Mbonde katika dakika ya 9 na Shiza Kichuya akaongeza la pili katika dakika ya 22. JKT walipata bao lao katika dakika ya 24 kupitia Saad Kipanga na mapumziko ikawa 2-1.



Katika kipindi cha pili, Mtibwa walitaka kuongeza bao, JKT wakataka kusawazisha lakini hakuna timu iliyofanikiwa kubadili lolote.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply