MWAMBUSI |
Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amelazimika kuondoka kikosini na kurejea kwao Mbeya baada ya kupata msiba.
Hata
hivyo, taarifa zinaeleza Mwambusi atarejea Dar Jumamosi, siku ambayo
Yanga itakuwa kazini kuivaa APR ya Rwanda katika mechi ya marudiano ya
Ligi ya Mabingwa ikiwa ni baada ya ushindi wa mabao 2-1 mjini Kigali,
Jumamosi iliyopita.
Mwambusi
alilazimika kuondoka juzi Jumatatu kwenda Mbeya kwa ajili ya kwenda
kumalizia msiba wa binamu yake ambaye alifariki wakati kikosi hicho
kikiwa nchini Rwanda wakati wakicheza na APR katika mchezo wa raundi ya
kwanza ambao Yanga ilishinda kwa mabao 2-1.
Mwambusi
amesema atalazimika kuwa nje ya kikosi hicho kwa siku kadhaa kutokana
na kusafiri kwenda Mbeya alikopatwa na msiba wa binamu yake.
“Kwa
sasa mimi nipo nje ya timu kwa siku kadhaa ambapo nimesafiri tangu
Jumatatu (juzi) nipo Mbeya huku nimekuja baada ya kupatwa na msiba wa
binamu yangu, nimekuja kumaliza msiba tu.
“Kila
kitu tayari kimeshafanywa maana alifariki wakati mimi nikiwa Rwanda
kwenye mchezo wetu dhidi ya APR ya nchini humo, nitakaa huku kwa siku
chache baada ya kupewa ruksa na viongozi wangu,”alisema Mwambusi.
SOURCE: CHAMPIONI
Hakuna maoni :