SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / SIMBA YATANGAZA KUMVUA ISIHAKA UNAHODHA, YAMSIMAMISHA MWEZI MZIMA.

ISIHAKA ( WA TATU KULIA) AKISHANGILIA NA WACHEZAJI WENZAKE


Klabu ya Simba, imetangaza kumsimamisha beki wake Isihaka Hassan kwa mwezi mmoja.

Pamoja na kumsimamisha, imetangaza kumvua unahodha msaidizi pale atakaporejea kundini. Hii ni kutokana na madai ya kumjibu kwa lugha isiyo ya kiungwana Kocha wake, Jackson Mayanja alipotaka kumpanga acheze katika mechi ya Kombe la FA dhidi ya Singida United.

Hayo yamesemwa leo na Msemaji wa Simba, Haji Manara wakati alipozungumzia suala la utovu wa nidhamu lililokuwa likimkabiri Isihaka ambaye alisimamishwa kwa muda usiojulikana.

Uamuzi huo wa kumsimamisha ambao ni sehemu ya uamuzi wa kamati ya utendaji, huenda ukasababisha Isihaka kuokosa Ligi Kuu Bara.

Siku Manara alipotangaza kumsimamisha Isihaka kwa muda usiojulikana, mshambuliaji wa Simba, Hamisi Kiiza aliandika mtandaoni kwamba mchezaji huyo alikuwa anaonewa na kuchafuliwa jina.

Lakini siku iliyofuata, isihaka alimuabisha Kiiza kwa kuomba radhi kutokana na kosa la kuzungumza kwa lugha isiyo ya kiungwana mbele ya kocha wake na wachezaji wengine.

Uongozi wa Simba ukampa onyo pia na kumtaka azikanushe habari hizo ambazo zilionekana zinalenga kutetea watovu wa nidhamu.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply