KIPA wa Arsenal Petr Cech atalazimika kuwa nje ya Uwanja kwa Wiki 3 mpaka 4 baada ya kuumia Musuli za Mguuni kwa mujibu wa Meneja wa Klabu hiyo Arsene Wenger.
Kipa huyo, ambae ndie nguzo kubwa ya Arsenal katika azma yao ya kutwaa Ubingwa kwa mara ya kwanza tangu 2004, aliumia Juzi wakati Arsenal inafungwa 2-1 na Swansea City Uwanjani Emirates.
Cech ataikosa Dabi ya Jumamosi huko White Hart Lane dhidi ya Tottenham Hotspur na Mechi nyingine muhimu ni marudiano ya Raundi ya 5 ya FA CUP na Hull City na marudiano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI huko Nou Camp dhidi ya Barcelona.
Hili ni pigo kubwa kwa Arsenal ambao wako Pointi 3 nyuma ya Timu ya Pili Spurs na Pointi 6 nyuma ya Vinara Leicester City katika Msimamo wa Ligi Kuu England.
Wenger amethibitisha kuumia vibaya kwa Musuli za Kipa huyo na pia kuelezea kuhusu Sentahafu Laurent Koscielny ambae pia nae aliumia kwenye Mechi hiyo hiyo na Swansea lakini yeye ataikosa Mechi na Spurs tu na kuweza kuwa fiti kuivaa WBA Wiki ijayo.
Hakuna maoni :