Mshambuliaji nyota wa KRC Genk, Mbwana Samatta usiku wa kuamkia leo, alitupia picha akiwatakia usiku mwema “watu wake wa nguvu”.
Samatta
ambaye tayari ameishaanza kuonyesha cheche zake kwa kufunga bao moja,
alitupia picha hiyo kwa lengo la kuwatakia washikaji, rafiki na wadau wa
soka usingizi mwema kwa ujumla.
Lakini picha hiyo ikatoa siri nyingine kabisa. Kwamba hivi; kumbe Samatta huwa analala na mpira wa soka.
Katika picha hiyo ukiangalia pembeni utaona mshambuliji huyo nyota Mtanzania utaona kuna mpira ukiwa umetulia.
Maana
yake, kuonyesha kweli ana hasira za kuendelea zaidi ya hapo, maana kama
Samatta analala na mpira, basi kweli hataki mchezo na kazi yake.
Hakuna maoni :