Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho Jumatano kwa
mchezo mmoja, ambapo Azam FC watawakaribisha Stand United katika uwanja
wa Azam Complex Chamazi.
Ijumaa mkoani Shinyanga katika uwanja wa Kambarage, wakata miwa wa
Kagera Sugar watakua wenyeji wa ndugu zao kutoka wakata miwa Mtibwa
Sugar kutoka Manungu Turiani.
Wikiendi Jumamosi na Jumapili ligi hiyo itaendelea kwa michezo
mitano kuchezwa katikwa viwanja mbalimbali nchini, jijini Tanga wenyeji
Coastal Union wakiwa wenyeji wa Simba SC katika uwanja wa Mkwakwani
jijini humo.
Majimaji FC itakua nyumbani katika uwanja wa Majimaji mjini Songea
kucheza na Mbeya City, huku chama la wana Stand United wakiwakaribisha
Ndanda FC katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Jumapili African Sports watakua wenyeji wa maafande wa jeshi la
magereza Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Mkwakwani jijii Tanga, huku
siku ya Jumatatu Mgambo Shooting wakicheza dhidi ya Toto Africans jijini
Tanga katika uwanja wa Mkwakwani.
TWIGA STARS KUWAFUATA ZIMBABWE IJUMAA
Timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Miguu “Twiga Stars”
inatarajiwa kusafiri siku ya Ijumaa kuelekea nchini Zimbabwe kwa ajili
ya mchezo wake wa marudiano wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa
Afrika kwa Wanawake zitakazofanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini
Cameroon.
Kikosi cha Twiga Stars kinaendelea na mazoezi katika uwanja wa
Karume chini ya kocha mkuu, Nasra Juma kujiandaa na mchezo huo muhimu
ili kuweza kusonga mbele katika hatua inayofuata.
Kuhusu maendeleo ya kambi, kocha Nasra Juma amesema vijana wake
wanaendela vizuri, wamekua wakiendelea na mazoezi tangu baada ya mchezo
wa awali na ana imani watafanya vizuri katika mchezo wa marudiano.
Twiga Stars inahitaji ushindi katika mchezo huo wa marudiano
utakaochezwa Jumapili, Machi 20 katika uwanja wa Rufalo uliopo jijini
Harare ili kuweza kufuzu kwa hatua ya pili ya michuano hiyo.
Hakuna maoni :