TAARIFA MUHIMU
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesikitishwa na taarifa za
upotoshaji za chombo kimoja cha habari ambacho mmoja wa watendaji
alipata fursa ya kuhudhuria mkutano mkuu kama mgeni mwalikwa
uliomalizika mwishoni mwa wiki jijini Tanga.
Katika hali inayotia mashaka, siku mbili kabla ya mkutano huo,
chombo hicho kiliripoti kuwa wajumbe walikuwa wanalalamika kwa
kutopelekewa nyaraka zinazohusiana na mkutano, wakati ukweli ni kuwa
nyaraka hizo zilitumwa tangu mwezi Novemba 2015 zikiwa ni sehemu ya
barua ya mwaliko wa kikao.
Hivyo isingewezekana mwaliko wa kikao
ukapokelewa na nyaraka zisiwepo. TFF inao ushahidi wa nyaraka hizo
kuwafikia wajumbe wa mkutano huo.
Katika toleo lake la leo chombo hicho kilidai TFF kupata hasara ya shilingi za kitanzania milioni 500.
TFF inaviomba vyombo vya habari kuacha kupotosha juu ya taarifa za
mkutano mkuu kuwa shirikisho lilipata hasara (loss) , TFF haifanyi
biashara yoyote mpaka kufikia kupata hasara, kilichotokea ni kuongezeka
kwa nakisi (deficit) katika bajeti ya mwaka 2014.
Matumizi yaliongezeka kutokana na kulipa madeni ambayo uongozi wa
sasa uliyakuta uliyosababisha hata basi la timu ya Taifa likamatwe,
kuwepo kwa michezo mingi ya timu za Taifa (Taifa Stars, Twiga Stars,
Serengeti Boys), gharama ambazo zilijumuisha kambi za maandalizi za timu
pamoja na safari.
Kwa kuwa TFF haifanyi biashara yoyote, matumizi yaliongezeka zaidi
ya bajeti iliyokuwa imeratajiwa na kufanya kuwepo na upungufu wa zaidi
ya milioni 490.
Aidha TFF imesikitishwa na taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo
vya habari mwishoni mwa wiki iliyopita, kuhusiana na suala la tiketi za
Elektroniki.
Ifahamike kwamba TFF ndiyo ilianzishwa matumumizi ya tiketi hizo
kabla hazijasitishwa na Serikali mwaka jana kutokana na kubaini
mapungufu katika utekelezaji.
TFF haijawahi kugomea kuwepo kwa mfumo huo wa ki elektorniki, na
kwa kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa
na Michezo wanaendelea na mazungumzo juu ya mfumo huo.
Vikao vinaendelea kati ya Wizara na TFF ili kuona njia gani itaweza
kutumika katika uendeshaji wa kuingia viwanjani kw aka kutumia mfumo wa
ki elektroniki na kesho kutakuwepo na kikao Wizarani kujadili mradi
huo.
TFF inatafakari juu ya hatua za kuchukua dhidi ya wanaotoa taarifa za upotoshaji huo.
Hakuna maoni :