Baada ya tambo nyingi kwa takribani wiki nzima, mechi ya wababe wa Yanga imemalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara ambayo ilipigwa kwenye Uwanja wa Taifa ilitawaliwa na kasi na upinzani mkali huku ubabe ukitawala kwa baadhi ya wachezaji.
Azam ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao lililotokana na beki wa Yanga, Juma Abdul kujifunga kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na straika Kipre Tchetche ambaye aliwatoka mabeki wa Yanga na kupiga krosi iliyojazwa wavuni na Abdul aliyetaka kuokoa.
Yanga ilisawazisha kupitia kwa Juma Abdul ambaye alipiga shuti kali baada ya kutokea piga nikupige katika lango la Azam.
Donald Ngoma ndiye aliyefunga bao la pili kwa Yanga kwa kichwa akiunganisha mpira uliopigwa na Amiss Tambwe.
Kuingia kwa bao hilo kuliongeza nguvu wa Yanga kushambulia zaidi lango la wapinzani wao, lakini kasi ilipopungua waliwapa nafasi Azam kusawazisha bao kupitia kwa nahodha wao, John Bocco.
Deus Kaseke alishindwa kuitumia nafasi nzuri katika dakika za lala salama baada ya kubaki yeye na kipa wa Azam, Aishi Munir lakini shuti lake likapanguliwa na kutoka nje.
Kutokana na matokeo.
Yanga imeendekea kukaa usukani kutokana na kufikisha pointi 47 sawa na Azam walipo nafasi ya pili wakiwa na pointi 47 ila wanatofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.
Hakuna maoni :