EVOUNA |
Straika
wa Al Ahly, Malick Evouna, ameshangazwa na jinsi Yanga walivyocheza
kwenye mchezo wao wa juzi Jumamosi wa Ligi ya Mabingwa Afrika na kusema
kuwa mchezo wao wa marudiano utakuwa mgumu.
Yanga
na Al Ahly zilikutana Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, kwenye
mchezo wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliomalizika kwa
sare ya 1-1 na zinatarajiwa kurudiana kati ya Aprili 19 na 20.
Mshambuliaji
huyo ambaye alicheza mechi hiyo kwa dakika tano akiingia akitokea
benchi kuchukua nafasi ya Moamen Zakaria, amesema kuwa kwa muda wote
aliokuwa benchi alikuwa akiusoma mchezo huku akishangazwa na Yanga
walivyokuwa wakicheza kwa kuonyesha upinzani, tofauti na alivyotarajia.
Alisema kuwa Yanga wana uwezo mkubwa wa kusonga mbele lakini amebaini kitu kitakachowaangusha ni kutojiamini kwao.
“Mchezo
ulikuwa mzuri kwa upande wetu lakini pia nawapongeza Yanga kwa jinsi
walivyocheza, wametupa upinzani tofauti na tulivyotarajia.
“Uwezo
wa kusonga mbele wanao, hatutawadharau hata kidogo kwenye mchezo ujao,
kuna kitu ambacho kinawaangusha, nilipokuwa benchi nilikuwa nawaona
wanacheza bila kujiamini, kama watajiamini wanaweza kutufunga,” alisema
Evouna.
Hakuna maoni :