• Manchester City (4-2-3-1): Hart 7, Maffeo 6.5, Stones 7 (Adarabioyo 60, 6)...

  • SALVATORY EDWARD Kiungo wa zamani wa timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kide...

  • Baada ya kikosi cha Mwadui FC kuchapwa kwa bao 1-0 katika mechi yao ya Lig...

  • Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeweka bayana kuwa, lipo kwenye mpango wa ...

SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / KUMBE TFF ILIWAPA AZAM FC KOMBE FEKI, SASA KUPEWA ORIGINAL.


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeweka bayana kuwa, lipo kwenye mpango wa kuwakabidhi kombe jipya la Ngao ya Jamii timu ya Azam kutokana na kukabidhiwa kombe ambalo halikuwa lenyewe.

Azam waliichapa Yanga kwa penalti 4-1 katika mchezo wa Ngao ya Jamii baada ya kumaliza dakika tisini kwa sare ya mabao 2-2, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar. 




  Msemaji wa TFF, Alfred Lucas ameliambia Championi Jumatano kuwa, waliwapa Azam ngao ambayo siyo yenyewe kutokana na kuchelewa kukamilika kwa utengenezwaji wa ngao halali ambalo walitakiwa kupewa.

“Lile kombe ambalo tuliwapa Azam siku ile walipocheza na Yanga kwenye Ngao ya Jamii halikuwa lenyewe, bali tulilitoa kwa ajili ya kuziba nafasi ya kombe halisi ambalo lilichelewa kuja kutokana na kutokamilika mpaka inafika siku ile, hivyo tukaona siyo vizuri bingwa akiondoka mikono mitupu.

“Tumepanga kuwabadilishia na kuwapa kombe lao halisi ambalo walistahili kupewa ambalo hili litakuwa na thamani halisi na mwonekano tofauti kabisa na lile ambalo tulilitoa awali,” alisema Alfred.

SOURCE: CHAMPIONI

«
Next
Alichokiongea Waziri Nchemba Baada yakufika Eneo Walipouwawa Askari Polisi Dar.
»
Previous
SCHWEINSTEIGER: SITAKI TENA KUCHEZA ULAYA, MAN UNITED NI KLABU YANGU YA MWISHO

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply