WANAUME wawili wanaoishi kama mume na mke (mashoga) nchini Afrika Kusini
wanasemekana kuwa watu wa kwanza katika ukanda huo na huenda duniani
kwa kuwa wazazi wa mapacha watatu, wawili wakiwa wanafanana, kwa kupitia
mtu mwingine aliyebeba mimba.
Wazazi hao ambao walikuwa majirani na mwanamichezo za zamani mlemavu,
Oscar Pistorius, walikutana na mtu waliyempatia mbegu zao wakati wa
mashitaka ya mauaji yaliyokuwa yanamkabili.
Christo na Theo Menelaou wamewachukua watoto wao nyumbani kwao mjini
Pretoria baada ya kukaa hospitali kwa wiki tatu za matatizo. Kutokana
na kuzaliwa kabla ya wakati wao, Julai 2, mapacha hao walijikuta maisha
yao yakining’inia kati ya uhai na kifo.
couple (1)Joshua alikuwa mtoto wa kwanza kuzaliwa kwa njia ya upasuaji
na ndiye alikuwa mzito kuliko wote akiwa na uzito wa kilo 1.8; Zoe
alifuatia akiwa na kilo 1.3 na Kate aliyekuwa na kilo 1.3 pia.
Watoto hao waliwekwa kwenye mashine za kuwasaidia kupumua hadi
walipokuwa na nguvu za kutosha na kuweza kuondoka katika hospitali ya
Sunninghill ya Johannesburg.
Waliondoka siku tofauti kwenda nyumbani, ambapo Joshua alikuwa wa kwanza
kuruhusiwa siku ya Julai 22, akafuata Zoe aliyeruhusiwa siku kumi
baadaye na Kate ambaye aliruhusiwa Agosti 4.
Christo Menelaou aliliambia shirika la utangazaji la Sky News: “Ukiwa
shoga, siku zote unafikiri kwamba haiwezekani ukawa mzazi hata kama una
upendo kiasi gani.
“Ni vigumu kupewa mtoto wa kuasili na kila mara tuliambiwa kwamba ni
wazazi wa kawaida tu ndiyo huruhusiwa. Pia hatukuweza kufikiri kwamba
tungempata mtu ambaye angekubali kubeba mbegu za mashoga.
Hata hivyo, mama mmoja mwenye watoto watatu, waliyekutana naye wakati wa
mashitaka ya Pistorious, alikubali kutubebea mbegu zetu.”
Sheria za Afrika Kusini kuhusu upandikizaji wa mbegu kwa watu wengine,
iliwataka wanaume wote wawili hao, mtu mwenye kubeba mbegu zao na mumewe
wasaini mkataba mbele ya jaji kusisitiza kwamba walikubaliana kwa hiari
katika jambo hilo na kwamba pasingekuwepo na kupeana fedha au kubeba
gharama zozote.
Wawili hao walikwenda kwenye benki ya mayai na kuchagua mayai ambapo
yai moja lilirutubishika na mbegu ya Christo na kuwekwa katika tumbo la
mbeba mimba na baadaye aliwekewa yai lililokuwa na mbegu ya Theo.
Baada ya wiki kumi za mimba hiyo, uchunguzi ulionyesha kwamba moja ya
mayai hayo yaliyorutubishika lilikuwa limejitenga na mbeba mimba alikuwa
ana mapacha watatu, wawili wakiwa ni wenye kufanana.
Wakati ambapo madaktari wengi waliwashauri wanaume hao kwamba mbeba
mimba huyo akatishe uhai wa mapacha wawili ili kutoa fursa ya mtoto wa
tatu kuendelea bila matatizo, hatimaye walimpata mtaalam wa masuala ya
watoto ambaye alisema angewasaidia jinsi ya kuhakikisha watoto hao
wanazaliwa salama.
Dk Heidra Dahms, ambaye ni mtaalam wa masuala ya watoto katika Hospitali
ya Sunninghill na aliyesimamia kuzaliwa kwa watoto hao, aliliambia
shirika la Sky News : “Ni jambo adimu sana. Sijawahi kusikia kitu kama
hicho hata siku moja.”
Watoto walikuwa ni wadogo mno, mapafu yao yalihitaji msaada wa ziada ili
kupumua na Theo alilazimikakulala kando ya kitanda hadi walipopata
nguvu.
Hata hivyo, wazazi hao wanakabiliwa na changamoto ya kumfanyia upasuaji
Zoe kutokana na kasorokwenye moyo, upasuaji ambao unahitajika kufanyika
katika kipindi cha miezi sita.
Pamoja na yote hayo, wawili hao wanasherehekea kuitwa ‘baba’, jambo ambalo hawakutegemea kamwe lingewezekana.
Hivi sasa wanaendelea kuwatunza watoto wao hao watatu nyumbani kwao kwa
msaada wa mayaya wawili usiku na mchana ambapo kila mtoto amefungwa
kidude kinachotoa sauti iwapo watashindwa kupumua.
Theo alisema: “Tunalazimika kuwasugua taratibu kwenye migongo yao au kutekenya vidole vyao ili kuwakumbusha kupumua.
“Tunajisikie tumebarikiwa sana,” alisema kwa furaha.
Tagged with: MATUKIO
Hakuna maoni :