SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / Unlabelled / HAYA TENA, MZUNGU WA MAJIMAJI NAYE ALIA WAMEPULIZIWA DAWA HARAMU VYUMBANI





 
KIKOSI CHA MAJIMAJI KILICHOPAMBANA HADI KUPANDA LIGI KUU BARA MSIMU HUU
Kocha Mkuu wa Majimaji ya Songea, Mika Lonnstrom raia wa Finland amesema vitendo alivyokutana navyo kwenye mchezo uliopita dhidi ya JKT Mgambo, bado vinamsumbua akili kwani anashangaa kwa nini vimetokea kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Wiki iliyopita, Kocha Mkuu wa Toto African, John Tegete alilalama kupulizwa kwa dawa kwenye vyumba vyao vya kubadilishia nguo wakati walipocheza na Coastal Union. Lakini meneja wa Uwanja wa Mkwakwani akadai walipulizia manukato tu.

 
SIKU MIKA  ALIPOWASILI NCHINI NA KUPOKELEWA NA NCHIMBI...
Majimaji wamekuwa wakilalamika kuwa walipuliziwa hewa yenye sumu katika vyumba vyao vya kubadilishia nguo wakati timu hizo zilipokutana kwenye Uwanja wa Mkwakwani, wiki iliyopita hali iliyowafanya waambulie kipigo cha bao 1-0.

Kocha huyo ameliambia gazeti hili kuwa alikuwa hajui kama Tanzania kunaweza kuwa na fitina za soka kiasi hicho, kwa kuwa amebaki na mshangao mkubwa kiasi cha kukosa majibu juu ya kile alichokishuhudia.

“Nimeshtushwa sana na hali ile, kama ligi ndiyo iko hivi, kwa kweli ni jambo la kushangaza, inapaswa TFF wawe wakali kwa kuzipa adhabu kali timu zinazofanya vitendo kama hivi. Lakini nimejifunza,” alisema Lonnstrom.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply