MATOKEO MECHI ZA LIGI YA
MABINGWA ULAYA USIKU HUU:
Real Madrid 4 – 0 Shakhtar Donetsk
Manchester City 1 – 2 Juventus
PSV 2 – 1 Manchester United
Galatasaray 0 – 2 Atletico de Madrid
Sevilla 3 – 0 Borussia Monchengladbach
Paris Saint-Germain 2 – 0 Malmo FF
VfL Wolfsburg 1 – 0 CSKA Moscow
Benfica 2 – 0 FC Astana
Real Madrid 4 – 0 Shakhtar Donetsk
Manchester City 1 – 2 Juventus
PSV 2 – 1 Manchester United
Galatasaray 0 – 2 Atletico de Madrid
Sevilla 3 – 0 Borussia Monchengladbach
Paris Saint-Germain 2 – 0 Malmo FF
VfL Wolfsburg 1 – 0 CSKA Moscow
Benfica 2 – 0 FC Astana

Juan
Mata akitupa mpira kwa hasira huku Anthony Martial akiwa ameshika uso
wake baada ya United kufungwa bao la pili na wenyeji PSV PICHA ZAIDI GONGA HAPA
TIMU za Manchester, England zimeanza vibaya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya zote kuchapwa usiku huu.
Manchester City wakiwa Uwanja wa nyumbani, Etihad wamepigwa 2-1 na Juventus katika mchezo wa Kundi D.
Licha
ya City kutangulia bao baada ya Giorgio Chiellini kujifunga dakika ya
57, lakini Mario Mandzukic akasawazisha dakika ya 70 na Alvaro Morata
akakifungua bao la ushindi Kibibi Kizee cha Turin dakika ya 81.
Mchezo
mwingine wa Kundi D, Sevilla ya Hispania imeanza vyema kwa ushindi wa
3-0 dhidi ya Borussia Monchengladbach ya Ujerumani Uwanja wa Sanchez
Pizjuan, mabao yake yakifungwa na Kevin Gameiro dakika ya 47, Ever
Banega dakika ya 66 yote kwa penalti na Yevhen Konoplyanka dakika ya 84.


Alvaro Morata (katikati) akishangilia na Juan Cuadrado na Paul Pogba baada ya kuifungia Juventus dhidi ya Man City PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Mashetani
Wekundu, Manchester United wameanza vibaya nao japokuwa walikuwa
ugenini, baada ya kuchapwa mabao 2-1 na PSV katika mchezo wa Kundi B
Uwanja wa Philips.
United
pia walitangulia kupata bao, mchezaji wake mpya Memphis Depay
akiiadhibu timu yake ya zamani dakika ya 41, kabla ya Hector Moreno
kusawazisha dakika ya 47 na Luciano Narsingh kufunga la pili dakika ya
57.
Mchezo
mwingine wa Kundi B, VfL Wolfsburg ya Ujerumani imepata ushindi
mwembamba wa 1-0 dhidi ya CSKA Moscow ya Urusi, bao pekee la Julian
Draxler dakika ya 40 Uwanja wa Volkswagen Arena.


Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia mabao matatu Real Madrid ikishinda 4-0 dhidi ya Shakhtar PICHA ZAIDI GONGA
Kundi C, Atletico Madrid wameanza vyema kwa ushindi wa 2-0 ugenini dhidi
ya Galatasaray nchini Uturuki, mabao ya Antoine Griezmann dakika ya 18
na 25 Uwanja wa Turk Telekom Arena, wakati Benfica ya Ureno imeshinda
2-0 nyumbani dhidi ya FC Astana, mabao ya Nicolas Gaitan dakika ya 51 na
Kostas Mitroglou dakika ya 62 Uwanja wa
da Luz.
Kundi
A; Paris Saint-Germain wameanza vyema pia kwa ushindi wa 2-0 nyumbani
dhidi ya Malmo FF, mabao ya Angel Di Maria dakika ya nne na Edinson
Cavani dakika ya 61 Uwanja wa Parc des Princes.
Mchezo
mwingine wa kundi hilo, Real Madrid wameifumua mabao 4-0 Shakhtar
Donetsk Uwanja wa Bernabeu, Mwanasoka Bora wa Dunia, Crisitano Ronaldo
akifunga matatu peke yake, dakika za 54, 63 yote kwa penalti na 81,
wakati lingine likifungwa na Mfaransa Karim Benzema dakika ya 30.

Winga wa zamani wa Real Madrid na Manchester United, Angel Di Maria akishangilia baada ya kuifungia PSG PICHA ZAIDI GONGA HAPA
MECHI ZA JUMATANO;
Hatua
ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itaendelea leo kwenye viwanja
nane, Valencia CFikiikaribisha Zenit St Petersburg Uwanja wa Mestalla,
Roma ikiikaribisha Barcelona Uwanja wa Olimpico, Olympiakos
ikiikaribisha FC Bayern Munich Uwanja wa Georgios Karaiskakis, KAA Gent
ikiikaribisha Lyon Uwanja wa Ghelamco, Dynamo Kyiv ikiikaribisha FC
Porto Uwanja wa Kiev Olympic, Dinamo Zagreb ikiikaribisha Arsenal Uwanja
wa Maksimir, Chelsea ikiwakaribisha Maccabi Tel Aviv Uwanja wa Stamford
Bridge na Bayer 04 Leverkusen ikiwakaribisha BATE Borisov Uwanja wa
BayArena.

Hakuna maoni :