Nahodha wa Mbeya City,
Juma Nyosso amerudia yaleyale baada ya kumdhalilisha nahodha wa Azam FC, John
Bocco.
Nyosso amempisha makalio
Bocco wakati wa mechi ya Ligi Kuu Bara ambayo Azam FC ilishinda mabao 2-1
kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam.
Nyosso aliwahi kumfanyia
hivyo mshambuliaji Elius Maguri wakati akiwa Simba, lakini akaomba radhi.
Lakini leo amerudia kwa makusudi kumfanyia hivyo Bocco hali iliyozua tafrani kubwa mwamuzi Martin Saanya naye akashiriki kuamua lakini akataka kujua ukweli wa jambo hilo baada ya malalamiko ya Bocco kutokana na kitendo hicho kibaya cha Nyosso ambaye ameonekana kamwe si mtu wa kubadilika.
Bocco alionekana
kuchukizwa na tukio hilo la Nyosso na kutaka kumvaa lakini wachezaji wa Azam FC
akiwemo Kipre Tchetche walifanya kazi ya ziada kuwatenganisha.
Hata hivyo, Nyosso
alionekana kuwa mkorofi akipinga kwamba hajafanya hivyo.
Baada ya kuona mambo ni
magumu, Nyosso ambaye ni nahodha alianza kumbembeleza Bocco ambaye kamwe
hakukubaliana na jambo hilo.
Mara ya kwanza, Blog hii
ilimuanika Nyosso akimfantia Maguri kitendo kama hicho, akaomba radhi lakini
TFF ikamfungia mechi nane.
Lakini yeye akaendeleza
kusema anajutia jambo hilo kabla ya leo kurejea kufanya upuuzi huo kwa mara
nyingine.
Benchi
la ufundi la Azam FC walipeleka ushahidi wa Nyosso kufanya hivyo kwa
mwamuzi wa akiba na baadaye kamisaa na sasa suala hilo litafika tena
TFF.
Hakuna maoni :