SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / Dr. Magufuli Tayari Keshapiga Kura, Chato......Kasema Matone ya Mvua Yamemnyeshea na Hiyo ni Ishara Kwamba Atashinda

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Magufuli amepiga kura katika jimbo la Chato mapema asubuhi hii na kueleza kuwa amepata dalili nzuri alipofika kwenye kituo hicho cha kupigia kura.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya kupiga kura, Dkt. Magufuli alieleza kuna dalili nzuri za ushindi kwa upande wake hasa baada ya matone ya mvua kuanza kudondoka punde alipofika kwenye kituo hicho.

Hata hivyo, Dkt. Magufuli hakutoa maelezo kuhusu matarajio yake na maoni yake kuhusu mchakato mzima wa kampeni pamoja na kutoeleza atayapokeaje matokeo ya aina yoyote.

Alito jibu la ufupi linaloashiria kuwa, “nitaeleza baada ya kuapishwa.”

Dkt. Magufuli aliwahimiza watanzania kuendelea kujitokeza kwa wingi kumchagua kiongozi wanaemtaka kwa ngazi zote za urais, ubunge na udiwani na kumtanguliza Mungu katika uamuzi wao.

“Mimi nimetimiza wajibu wagu kama raia, na nawashauri wenzangu wajihimu wakapige kura kwa kuwa hilo ndilo jukumu letu, wawachague marais, wabunge na madiwani.”

Aidha, Dkt. Magufuli alieleza kuridhishwa na mazingira ya zoezi la kupiga kura katika kituo hicho.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply