SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / KIIZA BADO SI SHWARI SIMBA SC, DAKTARI ASEMA…





MECHI ZIJAZO LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA Oktoba 3, 2015 Mgambo Shooting Vs Coastal  Majimaji FC Vs Mwadui FC Toto Africans Vs JKT Ruvu Stand United Vs Mbeya City Kagera Sugar Vs Prisons Kaitaba Oktoba 17, 2015
  Yanga SC Vs Azam Fc Majimaji FC Vs African Sports Mbeya City Vs Simba Sc Sokoine Ndanda FC Vs Toto Africans Stand United Vs Prisons Coastal Union Vs Mtibwa Sugar Mgambo Shooting Vs Kagera Sugar  Mwadui FC Vs JKT Ruvu
Majibu ya vipimo vya mshambuliaji wa Simba SC, Hamisi Kiiza 'Diego' yanatarajiwa kutoka leo


SIMBA SC leo inatarajiwa kujua itamkosa kwa muda gani, mshambuliaji wake tegemeo la mabao, Mganda Hamisi Friday Kiiza ‘Diego’.
  Kiiza aliumia mazoezini mapema wiki hii, Simba SC ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Stand United juzi, wakishinda 1-0, bao pekee la Joseph Kimwaga.
  Na Daktari wa Simba SC, Yassin Gembe ameiambia blog hii kwamba majibu ya vipimo vya Kiiza yatatoka leo.
  “Majibu yake (Kiiza) tutayapata Ijumaa na ndiyo tutajua anahitaji kupumzika kwa muda gani,”amesema Gembe, ambaye awali alikuwa Daktari wa timu nyingine ya Ligi Kuu, Mtibwa Sugar.
  Kiiza aliyueumia nyama za paja, hadi sasa ndiye kinara wa mabao wa Simba SC katika Ligi Kuu akiwa amefunga mabao matano katika mechi nne alizocheza.
  Baada ya kupoteza mchezo mmoja tu katika mechi tano, nyingine zote ikishinda, Simba SC itarudi kwenye Ligi Kuu Oktoba 17, itakapomenyana na Mbeya City mjini Mbeya.
  Lakini Ligi Kuu itaendelea kesho bila kuzihusisha Azam FC, Simba na Yanga SC, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Mgambo Shooting wakimenyana na  Coastal Union, Uwanja wa Majimaji, Songea wenyeji Majimaji FC wakiwakaribsiha Mwadui FC, Uwanja wa CC,m Kirumba,  Toto Africans wakiikaribisha  JKT Ruvu, Uwanja wa Kambarage, Shinyanga Stand United wakiikaribisha Mbeya City na Uwanja wa A.H. Mwinyi, Tabora, Kagera Sugar wakiikaribisha Prisons.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply