Baada ya kuisha kwa zoezi la kupiga Kura lililofanyika leo October 25 2015, najua kila Mtanzania atakuwa na hamu ya kuyapata matokeo.
Lakini zipo taarifa nilizozipata kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC ambapo hilo la utaratibu wa utoaji wa Matokeo limeguswa pia >>> “Tumeendesha
Uchaguzi wa Rais na Makamu ya Rais, shughuli imeendelea vema… Tumepata
taarifa na Zanzibar pia Uchaguzi umeendelea salama.” >>> Ramadhan K.Kailima, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, NEC.
Lakini kuna changamoto pia zilizojitokeza kwenye Uchaguzi huu >>> “Tulipata
tatizo kidogo maeneo ya Mkoa wa Rukwa, wakati gari linapeleka vifaa
kuna watu waliteka gari, wakalichoma moto na kuharibu vifaa vyote baada
ya kutokubaliana na malipo tuliyowapa… Tumekepeleka Karatasi za kupigia
Kura kwa ajili ya Kupigia Kura Rais pamoja na Mbunge wa kule lakini
Diwani tumeahirisha kwa sababu karatasi zilikuwa chache.”>
“Jeshi
la Polisi limekamata watu wote waliohusika na tukio hilo, tumepata
tatizo pia maeneo ya Dar es Salaam ikiwemo maeneo ya Kimara watu ndio
wanataka kuanza kupiga Kura kwa sababu Karatasi za kupigia Kura
ziliharibiwa” >>> Ramadhan Kailima.
Kuna baadhi ya maeneo pia Uchaguzi umechelewa kuanza leo, sababu ni hii hapa >>> “Baadhi
ya wadau toka mwaka 2010 walikataa Walimu wasitumike kusimamia
Uchaguzi, baadhi ya vijana tuliowachukua kufanya kazi hiyo walifanya
uharibifu wa vifaa vyote, imebidi tupeleke vifaa vingine na kazi ya
kupiga Kura imeanza japo kwa kuchelewa sana.”
Uchaguzi ukiisha huu ndio utaratibu wa kutolewa kwa matokeo ya Uchaguzi >>> “Matokeo
ya awali yataanza kutoka kesho saa tatu asubuhi, tutakuwa tunatoa kwa
awamu tatu au nne kwa siku… Itakuwa saa tatu asubuhi, saa sita, saa tisa
na saa 12 jioni…”
Na mshindi wa nafasi ya Urais atangazwa kwa utaratibu huu pia >>> “Tarehe
29 saa tatu asubuhi tutamtangaza mshindi wa nafasi ya Urais, tarehe 30
tunamkabidhi Cheti chake halafu tutamkabidhi Serikalini waendelee na
shughuli za kumuapisha.” >>>- Ramadhan Kailima
Hakuna maoni :