Mgombea
wa Udiwani jimbo la Mbagala Kuu, Dar es Salaam kupitia CCM, Yusuf Manji kesho
amepanga kufanya mkutano wake mkubwa kuzungumza na wakazi wa jiji hilo kubwa
nchini.
Manji
anatarajia
kufanya mkutano huo kwenye Viwanja vya Mbaghala Zakheem ambao utakuwa
mkutano wake wa kwanza kutangazwa kwani awali, mikutano mingi katika
mitaa ya Mbagala Kuu hakuwa akiitangaza lakini bado ilihudhuriwa na watu
wengi sana.
Taarifa
kutoka CCM Mbagala zimeeleza, mkutano huo utawajumuisha wanasiasa mbalimbali wa
eneo hilo pamoja na maeneo jirani.
“Manji
amekuwa akifanya mikutano sehemu mbalimbali katika mitaa ya Mbagala
Kuu, mkutano wa Jumapili pale Zakhem ni kwa ajili ya Wanadar es Salaam.
“Tunatarajia
kuwa na watu wengi huenda kuliko wale waliokuwa wakijitokeza katika
mikutano ya wagombea wa ubunge na hata urais,” alieleza mmoja wa
waandaaji wa mkutano huo kutoka CCM eneo la Mbagala.
Maandalizi
ya mkutano huo yameishaanza na bado haijajulikana Manji atazungumza
hasa jambo gani ingawa itakuwa ni sehemu ya kampeni zake.
Imani kubwa kwa Wanambagala kwa Manji imetokana na namna alivyopata mafanikio kupitia katika kampuni zake za Quality Group Ltd.
Lakini mafanikio makubwa akiwa na Yanga ambayo amefanikiwa kuiondoa katika migogoro na timu yake kuendelea kufanya vizuri.
Kwani tokea achukue kiti cha Uenyekiti wa Yanga, kikosi cha Yanga kimekuwa kikichukua ubingwa au kushika nafasi ya pili huku watani wao Simba wakiwa hawajashika nafasi ya pili au ubingwa kwa zaidi ya misimu mitatu sasa.
Hakuna maoni :