SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / MARIO GOETZE AUMIA, KUZIKOSA ARSENAL ZOTE 2!





GOETZEKIUNGO Mshambuliaji wa Bayern Munich Mario Goetze atakuwa nje ya Uwanja kwa Miezi Mitatu baada ya kuchanika Musuli za Pajani.

Goetze aliumia Ijumaa wakati Germany inafungwa 1-0 na Republic of Ireland huko Dublin katika Mechi ya Kundi lao la EURO 2016.

Kwenye Mechi hiyo, Goetze alitolewa nje ya Uwanja katika Dakika ya 35 na vipimo baadae vikathibitisha kwamba amechanika Musuli za Pajani.

Habari hizi pia zimethibitishwa na Klabu yake Bayern Munich ambayo pia imesema Mchezaji huyo bado yumo mikononi mwa Madaktari wa Timu ya Taifa ya Germany.

Germany, ambao wapo Kundi D, wanahitaji Pointi 1 tu wakicheza Nyumbani na Georgia Jumapili ili kufuzu kucheza Fainali za EURO 2016 Mwakani huko France.

Kuumia kwa Goetze ni pigo kubwa hasa kwa Bayern Munich kwani ameichezea Mechi 11 kati ya 12 Msimu huu na kufunga Bao 4 akiwafanya wawe Pointi 7 mbele kileleni mwa Bundesliga na pia kuwasaidi kushinda Mechi zao zote 2 za Kundi lao la UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Goetze sasa atazikosa Mechi muhimu zikiwemo zile 2 mfululizo za UEFA CHAMPIONZ LIGI dhidi ya Arsenal hapo Oktoba 20 na Novemba 4.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply