SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / MOURINHO AKEBEHI FAINI, AITA ‘FEDHEHA’, ASHANGAA ‘KUMSAMEHE’ WENGER!




WENGER-MOURINHOMENEJA wa Chelsea Jose Mourinho amesema Faini ya Pauni 50,000 aliyotwangwa na FA, Chama cha Soka England, ni fedheha.

Mourinho amepewa Adhabu hiyo ya faini pamoja na Kifungo cha Mechi 1 ambacho kimesimamishwa kwa Mwaka Mmoja kuchunguza mwenendo wake baada ya kupatikana na hatia ya utovu wa nidhamu kufuatia kauli yake kuhusu Refa Robert Madley mara baada ya kufungwa 3-1 na Southampton.

Mara baada ya Mechi hiyo, Mourinho alitamka Marefa wanaogopa kuwapa uamuzi Chelsea.

Mourinho ameeleza: “£50,000 ni fedheha, uwezekano wa kufungiwa Mechi 1 ni kitu cha kushangaza!”
Mourinho pia alimchimba Meneja wa Arsenal Arsene Wenger bila kumtaja jina alipogusia nini Wenger alisema mara baada ya kuchapwa 2-0 na Chelsea Mwezi uliopita.

Wakati huo, Wenger alidai Refa wa Mechi hiyo, Mike Dean, alikuwa ‘dhaifu’ na ‘asiefahamu’.
Mbali ya hilo, Wenger pia hakuadhibiwa na FA Oktoba 2014 wakati alipomsukuma Mourinho, aliekuwa eneo lake la ufundi, Chelsea ilipopambana na Arsenal Stamford Bridge.

Mourinho amelalamika: “Kuogopa ni Pauni 50,000, dhaifu na asiefahamu..ruksa. Unaweza kusukuma Mtu eneo lake la ufundi..si tatizo!”

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply