SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / PIQUE AZIDI KUZOMEWA SPAIN, CAZORLA ASONONEKA, RAMOS ASIKITIKA, DEL BOSQUE AAPA KUTOMTEM






PIQUE-BOOSKiungo wa Spain anaechezea Arsenal, Santi Cazorla, ambae Jana alipiga Bao 2 wakati Mabingwa hao wa Spain wakiifumua Luxembourg 4-0 kwenye Mechi ya Kundi C la EURO 2016 na kutinga Fainali huko France Mwakani, amesononeshwa na Mashabiki wa Spain kumzomea Beki wao Gerrard Pique.
Katika Mechi za hivi karibuni za Spain, Pique, Mchezaji wa Barcelona, amekuwa akizomewa na Mashabiki wa Spain na Jana huko Logrono Nchini Spain haikuwa tofauti.
Cazorla, akiongea baada ya Mechi ya Jana, amewasihi Mashabiki kuacha tabia hiyo.
Cazorla amenena: “Hii hali ya Pique si safi. Pique ni Mtu thabiti na yeye hubadilisha kuzomewa kuwa shangwe!”
Mwezi uliopita huko Oviedo, Uwanja wa Carlos Tartiere, Nchini Spain, Pique pia alizomewa wakati Spain inaifunga Slovakia 2-0 katika Mechi nyingine ya Kundi C la EURO 2016.
Chimbuko hasa la kuzomewa kwa Pique linatokana na msimamo wake wa kisiasa wa kutaka Jimbo la Catalan ambako Mji na Klabu ya Barcelona ilipo lijitenge.
Pia Mashabiki wa Real Madrid walikerwa mno na kejeli za Pique Msimu uliopita kwao na kwa Staa wao Cristiano Ronaldo walipokosa Mataji makubwa.
Hali hiyo ilimfanya hata Mchezaji wa Real Madrid kuwataka Mashabiki wa Spain wasitishe kuzomea huko kitu ambacho Kocha wa Spain, Vicente del Bosque, pia alitaka kiachwe.
Wakati huo Del Bosque alieleza: “Nadhani hali ya Pique si siasa bali ni upinzani wa Barca na Real. Akiwa na Timu ya Taifa amecheza Zaidi ya Mechi 70 kwa hali ya juu kabisa pamoja na zaidi ya Mechi 30 kwa Timu za Vijana. Lazima tumtetee. Nikimwacha Timu ya Taifa nitawapa ushindi wale wanaompinga wajione walikuwa na haki!”

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply