Penalti iliyofungwa na Raphael Alpha imezua
tafrani kubwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga wakati wa mechi hiyo ya
Ligi Kuu Bara.
Kiungo huyo wa Mbeya City alifunga penalty hiyo
ya dakika ya 90 baada ya Coastal Union kuongoza kwa muda wote.
Hali hiyo ilifanya mashabiki wa Coastal Union
kufanya vurugu kubwa ikiwa ni pamoja na kuharibu ubao wa kubadilishia
wachezaji, pia ripoti za mwamuzi wa akiba.
Polisi walilazimika kuingiza gari katikati ya
uwanja na kupambana na mashabiki hao kwa kupiga mabomu ya machozi.
Mashabiki hao waliendelea kurusha mawe wakiwapiga waamuzi ambao walipewa ngao ya Polisi kujilinda wakiwa katika gari la Polisi.
Hakuna maoni :