MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ufaransa, Karim Benzema jana alikuwa mchezaji pekee aliyecheza timu hiyo ikifungwa 4-0 na Barcelona Uwanja wa Santiago Bernabe katika La Liga kuripoti mazoezini.
Mfaransa
huyo aliibuka mazoezini viwanja vya Valdebebas kuungana na wachezaji
ambao hawakucheza El Clasico Jumamosi akina Casemiro, Alvaro Arbeloa and
na Lucas Vazquez.
Benzema na nyota wenzake wa Real, Gareth Bale na Cristiano Ronaldo walishindwa kutikisa nyavu za Barca mara moja juzi.
Luisa Suarez alifunga mabao mawili katika ushindi huo, wakati Neymar na Andres Iniesta kila mmoja alifunga bao moja, Real ikipoteza mechi ya kwanza ya La Liga nyumbani baada ya mechi 23.
Kikosi
kizima cha Real kinatarajiwa kufanya mazoezi kamili leo kujiandaa na
mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Shakhtar Donetsk


Hakuna maoni :