KIAPO! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mwigizaji matata Bongo, Aunt
Ezekiel ‘Mama Cookie’ kufunguka kuwa kamwe hatajihusisha kwenye ishu
yoyote ya sherehe inayomuhusu staa mwenzake Wema Sepetu ‘Madam’
isipokuwa kwenye tatizo la msiba unaomuhusu.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Aunt hakuhudhuria kwenye sherehe ya
kuzaliwa ya Wema, iliyofanyika mwishoni wa wiki iliyopita kwa sababu
shosti wake huyo wa zamani hajawahi kwenda kumuona mwanaye tangu
azaliwe.
“Aunt hakuweza kwenda kwa sababu bado anachukizwa na kitendo cha Wema
kutokwenda kumuona mtoto wake tangu amezaliwa kwa sababu hicho ndiyo
kilikuwa kitu muhimu maishani mwake hivyo hata yeye hawezi kwenda kwenye
ishu yake yoyote (Wema) ya furaha labda kutokee tatizo la kifo,”
kilisema chanzo hicho.
Alipotafutwa Aunt na kuulizwa kama kweli ndiyo wamefikia hatu hiyo na
Wema, alikiri kufikia hatua ya kutamka kauli hiyo kwani anashindwa
kumuelewa shosti wake huyo ana kitu gani moyoni ambacho kimemfanya
ashindwe kumtembelea tangu ajifungue.
“Nashindwa kumuelewa Wema sijui kuna kitu gani kikubwa kinachomfanya
ashindwe kumuona mwanangu na sisi tulikuwa marafiki. Siwezi kwenda
katika sherehe yake katika hali kama hii tuliyonayo labda kwa ishu ya
msiba, nitaennda,” alisema Aunt.Kwa upande wake Wema alipoulizwa
kuhusiana na suala hilo, hakuwa tayari kuzungumzia lolote.
Chanzo: GPL
Home
/
BURUDANI
/
KIMENUKA: Aunty Ezekiel Amchana Wema Sepetu Kuhusu Kutokwenda Kumuangalia Mtoto Wake Toka Azaliwe..Toa Kiapo Kikali
KIMENUKA: Aunty Ezekiel Amchana Wema Sepetu Kuhusu Kutokwenda Kumuangalia Mtoto Wake Toka Azaliwe..Toa Kiapo Kikali
Tagged with: BURUDANI
Hakuna maoni :