Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza viingilio
vya mchezo wa Jumamosi kati ya Tanzania dhidi ya Algeria utakaochezwa katika
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam bei ya chini kuwa ni shilingi elfu tano
(5,000) tu.
Tiketi za mchezo huo zitaanzwa kuuzwa siku ya ijumaa katika
vituo mbalimbali vinavyotumiwa na TFF kuuzia tiketi, ambapo kiingilio kingine
kitakua ni elfu kumi (10,000) kwa viti vya VIP B & C, huku kiingilio cha
elfu tano kikiwa ni kwa viti vya rangi ya Bluu, Kijani na rangi ya Machungwa.
Stars
kinatarajiwa kurejea nyumbani kesho Jumatano mchana kwa shirika la ndege la
Fastjet tayari kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo dhidi ya Algeria siku ya
Jumamosi.
Stars
iliyoweka kambi nchini Afrika Kusini imekua ikifanya mazoezi kila siku katika
uwanja wa Edenvale, ambapo mpaka sasa wachezaji wote wapo katika hali nzuri
hakuna majeruhi na kila mmoja yupo tayari kwa mchezo wa Jumamosi.
Aidha
Mkwasa amewaomba watanzania na wadau wote wa mpira wa miguu nchini kujitokeza
kwa wingi kuwapa sapoti ya kuwashangilia vijana katika mchezo dhidi ya Algeria
Jumamosi, kwani kutawafanya wachezaji kujisikia wapo nyumbani na kucheza kwa
nguvu zaidi.
Wachezaji
wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu walioshinda kombe
la Ligi ya Mabingwa mwishoni mwa wiki na klabu yao ya TP Mazembe wanatarajiwa
kuungana na wenzao kambini kesho jijini Dar ess alaam.
Hakuna maoni :