Ili kuipa hadhi na kuitangaza lugha yetu ya taifa, nashauri
rais wetu mpya atumie Kiswahili katika shughuli zote rasmi za kitaifa
na kimataifa. Cha msingi ni kuwa na wakalimani mahiri katika shughuli za
kimataifa. Hii itainua hadhi na heshima ya nchi yetu badala ya
kuendelea kuthamini lugha za kigeni.
Tumekuwa watumwa mno wa lugha ya
kiingereza mpaka kufikia hatua kudhani kuwa mtu anayeongea kiingereza
vizuri ndiye aliye elimika wakati si kweli.
Elimu ni uwezo siyo kuongea
kiingereza. Hiki kiingereza cha "izi, wozi, wea, kongrugesheni,
ameizingi, wati?, yu no, no problemu hakitusaidii kitu. Na kwa ujinga
wetu tunafundishana kwa lugha tusiyoijua vizuri matokeo yake watoto
wanafeli halafu tunawaona wajinga kumbe sera zetu ndio mbovu.
Wachina,
wakorea, wajerumani, wareno, wafaransa mbona wanatumia lugha zao na
wanapiga hatua kubwa sana katika uchumi na sayansi. Sisi na kiingereza
chetu cha kuombea maji tumefika wapi zaidi ya kutudhalilisha?
Maoni yangu haya hayana maana kuwa sitambui uwezo mkubwa wa
kiingereza alio nao dr. Nataka aendeleze pale mwenzake alipoachia
mwenzake, kwani alianza kwa kuhutubia kwa kiswahili kwenye mkutano wa AU
lakini baadaye akaacha.
Mimi nashauri Dr. sasa ajikite pamoja na mambo
mengi kuitangaza lugha ya kiswahili kimataifa kwa yeye mwenyewe kuitumia
badala ya kiingereza. Huwa naona viongozi wa nchi nyingine kama za
kiarabu pamoja na kuwa wanajua kiingereza lakini utakuta wanazaunguza
kiarabu na kisha wasiojua kutafsiriwa.
Wakalimani sasa hivi tunao wengi,
ni vizuri wakatumika vizuri kuikuza lugha yetu ya taifa. Ukweli ni kuwa
unapotumia lugha mama au lugha ya taifa una kuwa na uhuru na uwezo
mkubwa sana wa kujieleza na kuelezea kuliko unapotumia lugha za kigeni.
Kwa watanzania wengi lugha yetu ya mama ni kiswahili.
By Tulimumu
Hakuna maoni :