SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / BENZEMA ASIMAMISHWA KUICHEZEA FRANCE.


BENZEMA15Karim Benzema amesimamishwa kuichezea France hadi hapo uchunguzi kuhusu kuhusika kwake na Kesi inayomhusisha Mchezaji mwingi wa France, Mathieu Valbuena, kubanwa kutoa Fedha ili mkanda wake wa ngono usiwekwe hadharani.

Shirikisho la Soka la France limetangaza hatua hii dhidi ya Benzema, mwenye Miaka 27, na hili huenda likamfanya azikose Fainali za EURO 2016 zitakazochezwa Nchini France Mwezi Juni.
Benzema kwa sasa ndie Mfungaji Bora wa France akiwa na Bao 27 kwa Mechi 81.

Benzema amekanusha kuhusika kwake na Kesi hiyo ya kumchafua Mathieu Valbuena lakini Polisi wa France wamemburuta kwenye uchunguzi huo na sasa unasubiriwa uamuzi wa Jaji wa Mahakama kukata shauri kama Benzema anapaswa kushitakiwa au la.

Kuhusika kwa Benzema, ambae ni Straika wa Real Madrid, kunatokana na yeye kumwambia Valbuena kuwa upo Mkanda wa Video wa ngono unaomhusu na kumtaka aongee na wanaomiliki Mkanda huo ili kuepusha balaa.

Lakini Polisi wamemburuta Benzema kwenye Kesi hiyo kwa vile mmoja wa Watuhumiwa wake alimfahamu Benzema tangu utotoni.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply