Kocha
mpya wa Valencia Gary Neville ameibuka na kujibu tetesi zilizo zagaa
kwa watu wengi zinazomuhusisha yeye siku moja kurudi kuinoa Manchester
United ambayo kwa sasa ipo chini ya mholanzi Lois van Gaal.
Garry Neville amekanusha madai hayo ya yeye siku moja kuifundisha klabu ya Manchester United.
Legendary
huyo wa zamani wa United akicheza kama mlinzi wa pembeni na hahodha wa
kikosi hicho aliteuliwa kuwa kocha mkuu kuifundisha Valencia
inayoshiriki ligi ya Hispania La Liga mwanzoni mwa mwezi huu na wengi
wamekuwa wakimhusisha Neville kurithi mikoba ya Lois van Gaal ndani ya
Old Trafford baada ya mktaba wake kumalizika mwaka 2017.
Wakati
akifanyiwa interview na Sky Sports Garry Neville amesema, Old Trafford
siyo sehemu ambayo anaipa kipaumbele kwenye maisha yake ya kufundisha
soka wala haipo kwenye mipango yake ya baadae.
Alipoulizwa
kama anampango wa kurejea Old Trafford kama kocha Neville alisema;
“Hapana, mimi mwenyewe sijioni naifundisha Manchester United kabisa.
Nafahamu nataka kufanya nini kwenye maisha yangu na hilo halipo kabisa
kwenye akili yangu”.
Kwa
mtazamo wangu, hii ni hatua muhimu kwangu na inanipa uzoefu.
Nafahamu nahitaji mafanikio. Mafanikio yangu yatawafanya wachezaji
wafanikiwe na kuwa bora zaidi.
Neville
ambaye aliwahi kuwa kocha msaidizi wa England alichezea kipigo cha goli
2-0 kwenye mchezo wake wa kwanza alipokiongoza kikosi cha Valencia
dhidi ya Lyon kwenye dimba la Mestalla wakati wa mchezo wa klabu bingwa
Ulaya Jumatano iliyopita. Wababe hao wa Hispania wamedondokea kwenye
michuano ya Europa League.
Hakuna maoni :