SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / GARRY NAVILLE AIZUNGUMZIA ISHU YA KURITHI MIKOBA YA VAN GAAL OLD TRAFFORD



Kocha mpya wa Valencia Gary Neville ameibuka na kujibu tetesi zilizo zagaa kwa watu wengi zinazomuhusisha yeye siku moja kurudi kuinoa Manchester United ambayo kwa sasa ipo chini ya mholanzi Lois van Gaal.
Garry Neville amekanusha madai hayo ya yeye siku moja kuifundisha klabu ya Manchester United.
Nevill-2
Legendary huyo wa zamani wa United akicheza kama mlinzi wa pembeni na hahodha wa kikosi hicho aliteuliwa kuwa kocha mkuu kuifundisha Valencia inayoshiriki ligi ya Hispania La Liga mwanzoni mwa mwezi huu na wengi wamekuwa wakimhusisha Neville kurithi mikoba ya Lois van Gaal ndani ya Old Trafford baada ya mktaba wake kumalizika mwaka 2017.
Wakati akifanyiwa interview na Sky Sports Garry Neville amesema, Old Trafford siyo sehemu ambayo anaipa kipaumbele kwenye maisha yake ya kufundisha soka wala haipo kwenye mipango yake ya baadae.
Naville-4
Alipoulizwa kama anampango wa kurejea Old Trafford kama kocha Neville alisema; “Hapana, mimi mwenyewe sijioni naifundisha Manchester United kabisa. Nafahamu nataka kufanya nini kwenye maisha yangu na hilo halipo kabisa kwenye akili yangu”.
Naville-3
Kwa mtazamo wangu, hii ni hatua muhimu kwangu na inanipa uzoefu. Nafahamu nahitaji mafanikio. Mafanikio yangu yatawafanya wachezaji wafanikiwe na kuwa bora zaidi.


Neville ambaye aliwahi kuwa kocha msaidizi wa England alichezea kipigo cha goli 2-0 kwenye mchezo wake wa kwanza alipokiongoza kikosi cha Valencia dhidi ya Lyon kwenye dimba la Mestalla wakati wa mchezo wa klabu bingwa Ulaya Jumatano iliyopita. Wababe hao wa Hispania wamedondokea kwenye michuano ya Europa League.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply